ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 15, 2017

TAIFA STARS SARE NA RWANDA 1-1 CCM KIRUMBA MWANZA.

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani baada ya kukubali sare ya bao 1-1 dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza

Amavubi ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 17 kupitia kwa Domicique Nshuti dakika ya 18 kabla ya Himid Mao kuisawazishia Taifa Stars dakika ya 34 kwa mkwaju wa penalti.


Matokeo hayo yanaipa wakati mgumu Taifa Stars, kwani inatakiwa kushinda katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi ijayo jijini Kigali Rwanda.


Taifa Stars ikifanikia kushinda katika mchezo huo wa marudiano itasonga mbele katika hatua nyingine ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) zitakazofanyika Kenya mwakani.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.