ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 4, 2017

MWANAMKE AANGUA KILIO MBELE YA MAGUFULI WILAYANI SENGEREMA.




SENGEREMA: Rais John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela kuyafanyia kazi malalamiko ya mwanamke mmoja mkazi wa Sengerema aliyedai kunyanyaswa na kuvunjiwa nyumba yake.


Rais ametoa agizo hilo leo (Jumanne Julai 4) wakati akizindua mradi wa maji, wilayani Sengerema na kumtaka Mongela kuchukua namba ya simu ya mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rosemary Simon, ili atatuliwe tatizo lake.


Kabla ya Rais Magufuli kuchukua hatua hiyo, mwanamke huyo alikwenda mbele ya jukwaa alimoketi Rais, huku akilia kuwa ananyanyaswa na viongozi wa Chadema na kuwa wanataka kumbomolea nyumba yake, bila kufafanua ni kwa vipi.


“Mpe simu yako Mkuu wa Mkoa, halafu atakutafuta na wala usijali, nitamtuma Mkuu wa Mkoa  na haki yako itatendeka, nitalifanyia kazi suala lako,” amesema Rais.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.