ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 12, 2017

RAIS KENYATTA ASEMA KISIWA CHA MIGINGO NI MILKI YA KENYA, UGANDA BADO INADAI INAKIMILIKI.


  • Rais Kenyatta akihutubia wananchi katika eneo la Mbita, Kaunti ya Homa Bay Magharibi mwa Kenya, 2017,12,07
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kisiwa cha Migingo katika Ziwa Viktoria ni milki ya Kenya.
Kenyatta ameyasema hayo Jumatano ya leo katika eneo la Mbita, Kaunti ya Homa Bay na kuongeza kuwa, hivi sasa kunafanyika shughuli za kuchora mipaka ya kisiwa hicho.
Rais Kenyatta ambaye alikuwa ameandamana na Naibu wake, William Ruto ametoa tamko hilo katika hali ambayo Uganda pia inadai umiliki wa kisiwa hicho na mgogoro huo bado haujatatuliwa. Akiwa katika eneo hilo ambalo ni ngome ya kinara wa upinzani Raila Odinga, Rais Kenyatta amesema yeye kama Rais ana jukumu la kuwahudumia Wakenya wote bila kujali mitazamo yao ya kisiasa.
Kisiwa cha Migingo kinatajwa kuwa chenye idadi kubwa ya watu duniani kwa kuzingatia ukubwa wake ambao ni eneo lisilozidi ukubwa wa uwanja wa mpira, yaani ekari 0.49. Kisiwa hicho  kina nyumba zilizoezekwa kwa mabati, sababu ya kupewa jina “Iron Clad Island”.

Kisiwa cha Migingo (kulia) na Kisiwa cha Usingo katika Ziwa Viktoria
Samaki aina ya ‘Ngege’ ndio sababu kuu ya kisiwa cha Migingo kuvuma mno, na kuna kisiwa kikubwa cha Usingo karibu na Migingo ingawa hakuna anayethubutu kuishi hapo kwa imani kwamba kina mizimwi.
 
Mgogoro wa kisiwa cha Migingo ulianza mwaka 2008 baada ya wanajeshi wa Uganda kukivamia na kuwatimua Wakenya ingawa kimekuwa kikitambuliwa kuwa ni miliki ya Kenya.
Makubaliano ya awali kati ya Kenya na Uganda kuhusu kisiwa hiki yalifanywa 2016, na kwa sasa maafisa wa usalama kutoka nchi zote mbili wanalinda doria katika kisiwa hicho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.