ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 6, 2017

RAIS WA ALGERIA AMTAKA MKOLONI MFARANSA AIOMBE RADHI NCHI YAKE.


Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria kwa mara nyingine amemtaka mkoloni mkongwe wa Ulaya yaan Ufaransa aiombe radhi rasmi nchi yake kutokana na jinai kubwa alizowafanyia wananchi wa Algeria. 
Rais huyo wa Algeria alisema hayo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa nchi yake na kusisitiza kuwa, wananchi wa Algeria wanamtaka mkoloni wa jana yaani Ufaransa kuwaomba radhi rasmi kutokana na ukatili, jinai, mateso na masaibu mengi aliyowasababishia.
Kabla ya hapo pia Algeria ilikuwa imeitaka Ufaransa iwaombe radhi wananchi wa Algeria kutokana na ukatili na jinai alizowafanyia kwenye kipindi cha miaka 132 ya ukoloni wake katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria.
Hii ni katika hali ambayo rais mpya wa Ufaransa, Emanuel Macron aliitembelea Algeria mwezi Februari mwaka huu, wakati alipokuwa anagombea urais wa Ufaransa na kukiri katika ziara hiyo kwamba ukoloni wa nchi yake huko Algeria uliofanyika katika miaka ya kuanzia 1830 hadi 1962 ilikuwa ni jinai dhidi ya binadamu.
Zaidi ya watu milioni moja wa Algeria waliuliwa na wakoloni makatili wa Ulaya yaani Ufaransa katika vita vya ukombozi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Tangu wakati huo hadi hivi sasa, wananchi wa Algeria wamebakiwa na makovu ya jinai na ukatili waliofanyiwa na Wazungu hao wa Ulaya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.