ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 20, 2017

TANZIA: MWANAMUZIKI ROY MUKUNA KATUTOKA.

Mwanamuziki mkongwe, bingwa wa kupuliza saxophone, Roy Mukuna (pichani katikati) amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya taifa ya Muhimbiliji jijini Dar es Salaam.
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Enzi za uhai wake marehemu Roy Mukuna wa kwanza kushoto.
Roy Mukuna aliyetamba zaidi na bendi ya Maquis du Zaire (Maquis Original), alilazwa Muhimbili kwa siku kadhaa kufuatia kusumbuliwa na tatizo la ini. Kabla ya kupelekwa Muhimbili, Roy Mukuna alikuwa akiugulia nyumbani kwake Mburahati Barafu. ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Enzi za uhai wake marehemu Roy Mukuna wa tatu kutoka kushoto (mwenye nguo nyeupe full na kofia) akiwa na bendi ya Super kamanyola inayofanya kazi zake Villa Park jijini Mwanza.
Enzi za uhai wake marehemu Roy Mukuna katika upulizaji Saxophone.

Hadi kifo chake, Mukuna alikuwa rais wa bendi ya Super Kamanyola ya Mwanza ambayo ameitumikia kwa miaka mingi kabla ya kuzidiwa na kurejeshwa Dar es Salaam wakati wa mapumziko ya mwezi wa mtukufu wa Ramadhan mwaka huu. ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Aidha, kabla hajarejeshwa Dar es Salaam, mwanamuziki huyo alikuwa akitibiwa Mwanza ambapo kwa takriban miezi sita, hakuweza kuonekana kwenye jukwaa la Super Kamanyola. ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Mukuna aliyezaliwa Zaire (Congo) mwaka 1947, alizitumikia bendi za Super Matimila ya hayati Remmy Ongala na Tanza Muzika. "Msiba uko nyumbani kwake Mburahati Barafu jijini Dar es Salaam kwa taratibu za mazishi nasi kama uongozi tuko mbioni kuelekea humo kwaajili ya kukamilisha safari ya mwisho ya ndugu yetu" alisema meneja wa Villa Park Resort Ramadhan Maganga. 

#RIP Roy Mukuna. 

CC:- @jembenijembe @mbabavc @rama.maganga @jchameleone @jembefm 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.