ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 16, 2017

MBUNGE WA NYAMGANA AONESHA UFUNDI KATIKA FAINALI MABULA DRAFT CHAMPIONSHIP 2017

"Cheza mwanangu"Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula (kulia) akichuana na Mjumbe wa Baraza la Michezo la wilaya Nyamagana Kambarage, ikiwa ni mchezo wa kuashiria ufunguzi wa michuano hiyo, ambapo mbunge huyo aliibuka kidedea.
Michuano ya Nyamagana Draft Championship inafika tamati leo ambapo jumla ya timu 18 toka kata zote wilayani Nyamagana zimekutana ukumbi wa Ghand Hall hapa kuchuana.

Awali kabla ya fainali hizo kuanza kuchukuwa kasi mashabiki waliojitokeza wamefaidi mchezo wa ufunguzi uliokuwa na mbwembwe za aina yake kati ya Mbunge Stanslaus Mabula aliyetinga dimbani kucheza na Mjumbe wa Baraza la Michezo wilaya ya Nyaagana Bwana Kambarage ambapo tofauti na wengi walivyodhani kuwa ungekuwa mchezo uliopoza la-hasha mchezo ulikuwa na vijembe, ubishani na maneno ya kishabiki toka kwa pande zote mbili.

Hadi mwisho Mabula akaibuka kidedea.

Nyamagana Draft Championship ni mashindano ya mchezo wa draft yaliyoanzishwa takrinan miezi miwili iliyopita chini ya mwasisi wake Mbunge wa Jimbola Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula.
Macho mchezoni.
Mchezo uliovuta macho ya wengi ni huu wa ufunguzi:- Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula, akichuana na Mjumbe wa Baraza la Michezo la wilaya Nyamagana Kambarage, ikiwa ni mchezo wa kuashiria ufunguzi wa michuano hiyo, ambapo Mabula aliibuka kidedea.

Yakishirikisha kata zote 18 kila kata zilikuwa zikishindana kuhakikisha zinapata timu moja yenye wachezaji wa 4 wa 4 watakaocheza fainali.

Leo tarehe 16 July 2017 ndiyo fainali yenyewe kusaka bingwa.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula (katikati) akiteta jambo na Naibu Meya Jimbo la Nyamagana Bhiku Kotecha (kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo (kulia) katika ufunguzi wa fainali za Michuano ya Draft Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza.
 KAULI YA MBUNGE:-
Sote tunafahamu kuwa mchezo wa bao upo lakini hatujawahi kuufuatilia na kuutilia maanani kama michezo mingine ambayo hii leo twaiita mikubwa.

- Ukubwa wa mchezo unatokana na kuzingatiwa, kujengewa misingi na kupewa kipaumbele.
- Mchezo huu unahistoria kubwa sana kwa watanzania ni zao la mchezo wa bao ambao hutumia kete na mashimo.
Jimbo la Nyamagana limeamua kuufanya mchezo huu kuwa moja kati ya michezo ya kimashindano na hata kuufikisha ngazi ya mkoa, taifa na ikiwezekana kimataifa.

Afisa michezo Halmashauri ya jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko akitoa ratiba ya mashindano, vigezo na masharti.
Mashindano yanakamilika leo nayo hamasa imekuwa kubwa sana wachezaji wamejitokeza ingawa mwanzo walidhani ni masihala hivi lakini leo katika hatua ya mwisho mchezo umekuwa mkubwa hata zile kata ambazo hazikushiriki mwanzo, kwa kasi leo wanatamani kuingia kwenye hatua hii na kuwa sehemu ya washiriki.

Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni shilingi laki 4, kikombe na medali ya dhahabu.

Nafasi ya pili na watatu medali.

Lengo ni kuu ni kutengeneza wigo wa kuwa na michezo mingi na kutoa fursa kwa wenye uwezo na michezo hiyo ikiwa ni sambamba na kujenga urafiki, udugu, ushirika na kufahamiana.

"Wengi kutokana na ubize na harakati za maendeleo hatupati muda wa kukutana pamoja kutengeneza ushirika hivyo leo tunakutana hapa wadau wa kata 18 si kitu cha kawaida" Kisha akaongeza

"Kuna watu zaidi ya 100 hapa watu hawa wanakutana kwa mara ya kwanza kwa sababu walikuwa hawana sehemu ya kukutana, katika kukutana huko watu watabadilisha mawasiliano, mwenye hitaji mmoja anakutana na mwingine ambaye ni mtoa huduma na mwenye huduma atakutana na msajili wa watoa huduma hivyo tayari jamii itakuwa imerahisisha jambo hapo la kiaendeleo hata bila ya kutumia nguvu"


Mchakato wa upangaji wa timu chini ya kamati.
Vipute vimeanza.
Vipute mchezoni hapa ni Mbugani Vs Mabatini.
Mchuano na tafakari.
Mchezo wa awali Igogo Vs Luchelele.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.