ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 25, 2017

MAONESHO YA BIASHARA YA BIASHARA YA FAHARI YA GEITA YAZINDULIWA.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye ufunguzi wa maonesho ya Biashara ya Fahari ya Geita ambayo kwa mwaka huu yamefanyikia kwenye viwanja vya Kalangalala ikiwa ni awamu ya Pili tangu kuanza Mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meje Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisalimiana na meneja mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw,Manase Ndoroma wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya maonesho.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meje Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisalimiana na kuteta jambo na Meneja wa NSSF Mkoani Geita  Shabaan Mpendu , wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya maonesho.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meje Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,akisaini kitabu cha mahudhulio kulia  ni mwenyekiti wa maandalizi ya  maonesho ya fahari ya Geita Raphael Siyantemi na Kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita Leornad Kiganga Bugomola.
mwenyekiti wa maandalizi ya  maonesho ya fahari ya Geita Raphael Siyantemi,akitoa utambulisho kwa mgeni rasmi na kuwashukuru wafadhili ambao wamejitolea kwa moyo mkunjufu kudhamini maonesho hayo wakiwemo kituo cha radio cha Storm fm,Mgodi wa dhahabu wa Geita,NSSF,Clouds media Group WAJA na wengineo.


Meneja mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw,Manase Ndoroma ,akiwawakilisha wafhadhili ambao wamehusika kufadhili maonesho hayo ya Biashara pamoja na kusisitiza wao kama Mgodi wataendelea kushirikiana na wadau wa maonesho hayo kwa kutoa ufadhili pamoja na kushiriki kwa kila mwaka.

Mchezi Ngoma za asili kutoka Wilayani Chato akitoa Burudani wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Biashara Mkoani Geita.

Msanii wa  vichekesho ambaye anajulikana kwa jina la Mfupi kwenda chini akituzwa wakati alipokuwa akitoa Burudani kwenye maonesho.

Kikundi cha Vichekesho cha Futuhi wakitoa Burudani .

Brother K maarufu kwa jina la Tajiri wa Kigoma  wa kikundi cha Futuhi akiendelea kufanya yake.

Baadhi ya mabanda ambayo yapo kwenye maonesho.


Mgeni Rasmi,ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Meje Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,akipatiwa maelezo na  afisa wa Polisi Bi,Esnart Magoti wakati alipotembelea Banda la Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama Barabarani.

Afisa Masoko na uhusiano wa NSSF Makao makuu,Bi Aisha Sango akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi  namna ambavyo wamekuwa wakitoa huduma na kusajili baadhi ya watu ambao wanajiunga na mfuko wa Bima ya Nssf.

Meneja wa NSSF Mkoani Geita  Shabaan Mpendu ,akiongezea juu ya mfuko wa NSSF ambavyo wameendelea kuboresha huduma za mfuko huo siku hadi 

Lango ka Kuingilia kwenye maonesho ya Bishara ya Fahari ya Geita.


Picha Zote na Joel Maduka wa Maduka Online.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.