ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 31, 2017

KOREA KASKAZINI YAIONYA MAREKANI ISITUMIE NJIA YA KIJESHI NA VIKWAZO DHIDI YAKE.


Serikali ya Korea Kaskazini imeionya Marekani isitumie njia za vikwazo zaidi wala za kijeshi dhidi ya Pyongyang.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imetoa taarifa kuionya Washington kwamba, iwapo itatumia vikwazo zaidi dhidi yake au njia ya kijeshi, basi itakabiliwa na jibu kali zaidi. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema kuwa, majaribio ya kombora la balestiki yaliyofanywa hivi karibuni na Pyongyang ni onyo kwa Marekani.
Ijumaa iliyopita, Korea Kaskazini ililifanyia majaribio kombora lake la balestiki la kuvuka mabara kwenda katika maji ya Japan. Baada ya jaribio hilo, Kim Jong-un, kiongozi wa nchi hiyo alitangaza kuwa jaribio hilo limethibitisha kwamba, sasa ardhi yote ya Marekani inaweza kulengwa kwa makombora ya Pyongyang.
Kombora la kuvuka mabara la Korea Kaskazini.
Kwa mara kadhaa Korea Kaskazini imekuwa ikisisitiza azma yake ya kuendelea kujiimarisha kijeshi kwa silaha za nyuklia hadi pale Marekani na washirika wake watakapositisha vitisho dhidi yake. 

Wakati huo huo, habari zinaarifu kwamba raia wa Korea Kaskazini wamepatwa na ghururi hasa baada ya serikali ya nchi hiyo kufanya jaribio la kombora jipya siku ya Ijumaa iliyopita. Televisheni ya APTN imetangaza kuwa, baada ya jaribio hilo wakazi wa miji kadhaa walikusanyika katika viwanja mbalimbali na kushangilia hatua hiyo ambayo wameitaja kuwa ni ushindi mkubwa dhidi ya Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.