ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 15, 2017

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA RWANDA AIFANANISHA PEACH YA UWANJA WA CCM KIRUMBA NA MATUTA YA VIAZI.

Kushindwa kupata ndege ya kuunganisha moja moja toka Kigali nchini Rwanda hadi Mwanza, kunasababisha wachezaji wa Rwanda Amavubi, kuwasili jijini humo kwa mafungu.

Ni wachezaji 11 na kocha wao ndiyo wamewasili mkoani hapa majira ya saa 2 asubuhi kwaajili ya kipute hicho huku wengine 7 wakisalia jijini Dar es salaam wakitaraji kutinga jijini hapa na ndege ya usiku.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Antoine Hey analazimika kulishushia lawama shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kwa kupanga mchezo huo CCM Kirumba badala ya Uwanja wa Taifa Dar es salaam na kisha anaongeza malalamiko yake kwa shirikisho kushindwa kutumia fair play kulisogeza mbele pambano hilo dhidi ya Taifa Stars.

 Kocha Hey ameiponda peach ya dimba la CCM kirumba akiifananisha na matuta ya viazi lakini yote tisa TFF wanasema mchezo uko pale pale.

Mimi ni Albert G Sengo wa Gsengo Tv.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.