ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 11, 2017

KIJANA WA IRAN ASHINDA TUZO YA UVUMBUZI BORA WA DUNIA MWAKA 2017.


Khalil Nazari, mvumbuzi na mtafiti wa Kiirani amefanikiwa kushinda tuzo maalumu na medali ya fakhari ya mashindano makubwa ya uvumbuzi ya INPEX nchini Marekani.
Uvumbuzi wa Khalil Nazari umehusisha uhuishaji majani wa 'HL' badala ya utumiwaji mafuta ya Mulch kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa hewa mijini. Mashindano hayo yaliwahusisha wavumbuzi 800 kutoka nchi 40 za dunia ambapo kijana huyo wa Iran ameweza kupata tuzo na medali ya fakhari ya INPEX nchini Marekani mwaka huu wa 2017 na hivyo kuweza kupeperusha bendera ya nchi yake.
 Barabarani vyombo vya usafiri vimekuwa chanzo kikuu katika uchafuzi wa mazingira.

 Kaya zilizo kandokando au pembezoni mwa vyanzo vya maji nako ni hatari.

 Athari za uchafuzi wa mazingira na viumbe vilivyomo majini.

 Uvuvi unapogeuka kuwa kero.

 Viwanda na uzalishaji sumu nayo wakiielekeza kwenye vyanzo vya maji.

Taka ngumu, sugu.

Uchafuzi wa mazingira duniani
Mashindano ya wavumbuzi ya INPEX nchini Marekani, yanahesabika kuwa mashindano makubwa ya uvumbuzi duniani. Jamhuri ya Iran imekuwa ikishika nafasi mbalimbali za kielimu katika maonyesho na mashindano tofauti duniani katika miaka ya hivi karibuni na hivyo kuifanya ihesabike kuwa mfano wa kuigwa kati ya nchi zinazoinukia kielimu na kimaendeleo.

 Mafanikio hayo ya Iran yanapatikana huku taifa hili likiwa limewekewa vikwazo vya kila upande na madola ya Magharibi hususan Marekani kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.