ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 24, 2017

IMF: MAFUTA YAUPAISHA UCHUMI WA IRAN


Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umeripoti kuwa ukuaji wa kiuchumi wa Iran umekuwa na taathira chanya kwa uchumi wa eneo la Mashariki ya Kati. 
IMF Imeripoti leo kuwa utendaji mzuri katika mwaka uliopita wa 2016 katika eneo la Mashariki ya Kati ulikuwa ni matokeao ya kuongezeka pakubwa ukuaji wa kiuchumi wa Iran kwa zaidi ya asilimia 6.5. Mfuko wa Fedha wa Kimataifa umeripoti pia kuwa uchumi wa Iran umekuwa kutokana na kuongezeka kiwango cha uzalishaji wake wa mafuta.

Kiwango cha uzalishaji wa mafuta wa Iran kwa utaratibu wa miaka.

IMF aidha imetabiri kwamba ukuaji wa kiuchumi wa Saudi Arabia mwaka huu utaporomoka hadi sifuri. Benki ya Dunia pia huko nyuma ilitoa ripoti inayoashiria kukua vyema uchumi wa Iran na kulitaja ongezeko hilo kuwa  zaidi ya asilimia sita.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.