ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 21, 2017

GAZETI LA GUARDIAN: TRUMP ANAELEKEA KUISAMBARATISHA MAREKANI.


Gazeti la The Guardian linalochapishwa mjini London, Uingereza limeandika kuwa, hatua za Rais Donald Trump wa Marekani zinaisambaratisha nchi hiyo.
Mtandao wa habari wa gazeti hilo sambamba na kuashiria kipindi cha miezi sita tu tangu aingie madarakani rais huyo wa Marekani, limeandika kuwa, ahadi za kiuchumi na kibiashara za Trump hazina mustakbali wowote wa kutekelezeka. Aidha limeandika kuwa hadi sasa Trump hajaweza kutekeleza ahadi zake hizo kuhusiana na kuufanyia mabadiliko mfumo wa fedha wa Marekani. 

Gazeti la  The Guardian la nchini uingereza
Gazeti hilo limezungumzia pia hatua ya Marekani ya kujiondoka katika mkataba wa hali ya hewa wa mjini Paris, Ufaransa na kuandika kuwa, katika kipindi cha chini ya miezi sita pekee, Trump ametupilia mbali mipango muhimu ya mtangulizi wake, Barack Obama hususan katika uga wa mazingira. 

Pia limeitaja amri ya Rais Donald Trump dhidi ya uhajiri kuwa ni hatua ya tatu ya kuisambaratisha Marekani na kufafanua kuwa, amri hiyo inayowazuia raia wa mataifa sita ya Kiislamu kuingia nchini Marekani, imeibua mgogoro na vurugu katika viwanja vya ndege vya nchi hiyo hasa kwa kuwa inawatenganisha watu wa familia moja.


 Umasikini ulivyoongezeka nchini Marekani.
Likizungumzia udiplomasia wa kigeni wa Rais Trump, The Guardian limeandika kuwa, kitendo cha rais huyo kufanya mahusiano na urafiki na viongozi madikteta kama vile Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudia, ni hatua nyingine inayodhoofisha stratijia ya Marekani duniani na kwa mujibu wa utafiti mpya wa kituo cha uchunguzi cha Pew, kati ya nchi 37 kulikofanyika uchunguzi huo, ni asilimia 22 tu ya watu walionyesha kumuunga mkono Trump katika masuala ya kimataifa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.