ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 10, 2017

DEREVA NA KONDAKTA WA BUS LA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI WILAYANI MISUNGWI.
KWAMBA TAREHE 06.07.2017 MAJIRA YA SAA 12:30HRS KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA KIJIJI CHA MISUNGWI KATA NA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI AMBAO NI DEREVA NA KONDAKTA WA GARI LENYE NAMBA T.574 AZU AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS , WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.SUDI YUSUPH MIAKA 35, DEREVA WA BUS LA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS, MKAZI WA BUZURUGA –MWANZA NA 2.BONIPHACE MASHAURI, MIAKA 52, KONDAKTA WA BUS LA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS, MKAZI WA MUSOMA – MARA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA “MIRUNGI” KIASI CHA MABUNDA 112, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

AWALI POLISI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA BUS TAJWA HAPO JUU LINALOFANYA SHUGHULI YA KUSAFIRISHA ABIRIA KUTOKA MUSOMA KWENDA DODOMA LINAJIHUSISHA PIA NA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA   (“MIRUNGI”).  AIDHA BAADA YA ASKARI KUPATA TAARIFA HIZO WALIWEKA MTEGO, NDIPO JANA TAREHE TAJWA HAPO JUU BUS HILO LIKIWA LINATOKEA MUSOMA KWENDA DODOMA LILIPOFIKA KIJIJI CHA MISUNGWI ASKARI WALILISIMAMISHA KISHA  LIKAFANYIWA UPEKUZI NA KUKUTWA LIKIWA LIMEBEBA  MIRUNGI AMBAYO NI KUNDI LA MADAWA  YA KULEVYA KIASI CHA BUNDA 112, YALIYOKUWA YAMEHIFADHIWA NDANI YA MABEGI KISHA KUWEKWA NDANI YA BUTI YA GARI.

MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE NI UTINGO WA GARI HILO AMETOROKA, JUHUDI ZA KUMTAFUTA BADO ZINAENDELEA. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WAWILI WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UCHUNGUZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA UTUMIAJI, UUZAJI NA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KATIKA MKOA WA MWANZA BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO HUSUSANI WAMILIKI WA MABASI KUACHA KABISA TABIA YA KUJIHUSISHA NA USARISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KWANI NI KOSA LA JINAI NA ENDAPO GARI LITAKAMATWA  HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHULIWA DHIDI YA MWENYE MALI. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WAHALIFU NA UHALIFU MAPEMA ILI WATUHUMIWA WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.