ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 13, 2017

CUF LIPUMBA WATOA ONYO KALI CHADEMA.

Chama cha wananchi CUF upande wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa Chama hicho Prof Ibrahim Lipumba umesema hautokuwa tayari kuona vyama vingine vinaingilia kati mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho baina ya kambi hiyo na ile ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad.

Kutoka ofisi za CUF Buguruni, Kaimu katibu mkuu anayetambuliwa na upande wa Lipumba ambaye ni mbunge wa Kaliuwa Magdalena Sakaya anasema amekwisha andikia vyombo vya dola kuwahakikishia kuwa hakuna vurugu zitakazotokea kama zinavyodaiwa kuandaliwa na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.