ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 28, 2017

BINTI WA MIAKA 17 ABAKWA KWA AMRI YA BARAZA LA KIJIJI, KISA? KAKA YAKE KABAKA.


Polisi ya Pakistan imeamuru kutiwa nguvuni wajumbe 20 wa Baraza la kijiji kimoja cha katikati mwa nchi hiyo baada ya wajumbe hao kutoa hukumu ya kubakwa na kunajisiwa binti mwenye umri wa miaka 17 ili kulipiza kisasi cha uhalifu kama huo uliofanywa na kaka yake. 
Suala hilo limefichua zaidi hali inayotawala mfumo wa kikabila nchini Pakistan. Kamanda wa Polisi ya eneo hilo, Saliim Khan Niyazi amesema kuwa, msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 alibakwa na kunajisiwa katika mji wa Multan katika jimbo la Punjab.
Baraza la kijiji hicho liliamuru msichana huyo abakwe ili kulipiza kisasi cha kitendo kilichofanywa na kaka yake cha kumbaka msichana mwingine katika eneo hilo. Msichana huyo alikamatwa na kubakwa mbele ya wazazi wake.

Mabaraza ya vijiji yanatambuliwa kuwa ni mbadala wa mahakama dhaifu za Pakistan ambazo huchelewesha kesi zinazowasilishwa huko kwa miaka mingi. Maamuzi ya mabaraza hayo yanayotegemea ada za kikabila, yanakubaliwa na wakazi wa maeneo ya vijijini, ingawa hayatambuliwi rasmi na serikali ya Pakistan.
Kamada wa Polisi, Saliim Khan Niyazi amesema mkuu wa baraza hilo lililotoa hukumu ya kubakwa msichana huyo na wajumbe wengine 20 wametiwa nguvuni na kwamba mtuhumu mkuu ametoroka.
Mkuu wa jimbo la Punjab, Shahbaz Sharif ameliamuru jeshi la polisi kuwasaka na kuwakamata wajumbe wote wa baraza la kijiji hicho

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.