ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 31, 2017

AFISA WA UCHAGUZI KENYA ATESWA NA KUUAWA KABLA YA UCHAGUZI.


Afisa wa ngazi ya juu wa uchaguzi wa Kenya leo amekutwa ameuawa siku tatu baada ya kutoweka. Hayo yameeleawa na maafisa uchaguzi wa Kenya.
Kuuliwa kwa afisa huyo kumezidisha wasiwasi na hofu juu ya uwezekano wa kutokea machafuko kabla ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.

Chris Msando aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Teknoloijia  katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) aliteswa kabla ya kuuawa. Hayo yameelezwa na kitengo hicho cha IEBC.
Eneo la Nguriunditu ulipokutwa mwili wa Afisa  wa IEBC aliyeuawa kikatili.
Wakenya ambao walikumbwa na ghasia nchini mwao baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Jumanne wiki ijayo wataelekea katika masanduku ya kupigia kura kumchagua Rais mpya, wabunge na magavana.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, Wafula Chebukat amesema kuwa hakuna shaka kwamba afisa huyo aliteswa na kisha kuuliwa. Amesema swali linaloulizwa sasa ni kwamba nani aliyemuuwa afisa huyo na kwanini?
Chebukati ameiomba serikali kutoa ulinzi kwa wajumbe wote wa tume hiyo ili kuhakikisha kuwa Wakenya wanakuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.