ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 3, 2017

WATOTO 15 WAMEKUFA BAADA YA CHANJO YA SURUA KWENDA MRAMA SUDANI YA KUSINI.

Watoto 15 wamepoteza maisha Sudan Kusini baada ya kampeni ya chanjo ya surua ya tarehe 10 hadi 14 Mei kwenda mrama.

Shirika la Afya Duniani WHO limesema limesikitishwa na taarifa ya vifo vya watoto 15 katika kijiji cha Nachodokopele Mashariki mwa Kapwete nchini Sudan Kusini, vinavyohusiana na kampeni ya chanjo ya surua ya tarehe 10 hadi 14 Mei kwenda mrama.
Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Alhamisi na WHO, Shirika la Kuhudumia watoto UNICEF na Wizara ya Afya ya Sudan Kusini ,baada ya uchunguzi wa kina wa vifo hivyo imebainika kwamba kampeni hiyo ya chanjo ilihusika na vifo vya watoto hao. Tariki Jasarevic msemaji wa WHO amebaini kuwa makosa ya kibinadamu yamechangia vifo hivyo.
Mtoto akichanjwa.
Amesema sababu kuu vifo hivyo ni kutumiwa wahudumu wasio na ujuzi ambao hawakupata mafunzo ya jinsi ya kutoa chanjo kwa viwango vinavyotakiwa na kutofuatiliwa na kusimamiwa ipasavyo utoaji chanjo hiyo.
Ameongeza kuwa bomba moja la sindano lilitumika kutoa chanjo kwa siku zote nne badala ya kutupwa baada ya kutumika mara moja jambo ambalo ni kinyume na viwango vya afya na usalama vya WHO, na kusababisha dawa ya chanjo kuchanganyika na vitu visivyotakiwa na kuwadhuru watoto hao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.