ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 14, 2017

WAMISRI WAANDAMANA KUPINGA KUPEWA SAUDIA VISIWA VIWILI VYA NCHI YAO.

Wananchi wa Misri wamefanya maandamano katika mji mkuu Cairo, kulalamikia uamuzi wa Bunge la hiyo nchi hiyo wa kuidhinisha kupewa Saudi Arabia visiwa viwili vya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika vya Tiran na Sanafir.

Huku wakipiga nara zenye ujumbe dhidi ya serikali ya Rais Abdul Fattah al-Sisi wa nchi hiyo, waandamanaji hao wamesikika wakisema "Tumechoka na utawala wa kijeshi".

Hamdeen Sabahi, mmoja wa wanaharakati hao amesema kukabidhiwa visiwa hivyo kwa Saudia hakutakuwa na tija nyingine ghairi ya kupanua wigo na satua ya Israel katika eneo hilo.

Hapo jana, Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge la Misri ilipasisha kwa kura 35 dhidi ya 8, uamuzi wa serikali ya Cairo wa kuukabidhi utawala wa Aal-Saud visiwa vyake viwili vya Tiran na Sanafir.

Polisi ikikabiliana na waandamanaji kwa vitoa machozi jijini Cairo.
 Wakili na mwanaharakati mtajika wa Misri, Amr Khashab amesema katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa: Tupo tayari kufa au kukamatwa kwa ajili ya kutetea ardhi yetu.
 
Mapema mwezi huu, shakhsia na wasomi 1500 wa Misri walitangaza rasmi upinzani wao kwa uamuzi wa serikali ya nchi hiyo wa kutaka kuipa Saudi Arabia visiwa hivyo viwili kupitia muafaka uliofikiwa Aprili 8 mwaka jana, kati ya Rais Sisi na Mfalme Salman wa Saudia alipoitembelea Misri.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.