ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 19, 2017

WAASI 12 WA MAIMAI WAUAWA DRC.

Watu 13 wameuawa katika mapigano yaliyozuka baina ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi, mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi la nchi hiyo limetangaza kuwa, waasi 12 wa Maimai na mwanajeshi mmoja wa serikali wameuawa katika mapigano yaliyotokea jana baina ya pande hizo mbili kwenye eneo la Kabasha la kusini mashariki mwa mji wa Beni wa Kivu Kaskazini.
Taarifa ya jeshi hilo imeongeza kuwa, waasi wa Maimai walishambulia eneo la Kabasha katika barabara ya Beni-Butembo na kuwalazimisha wanajeshi kujibu mshambulizi hayo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashambulizi baina ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa Maimai katika eneo la Kabasha yalianza tangu siku ya Jumatano.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Asasi za kijamii za nchi hiyo zimesema kuwa, takriban wakazi wote wa eneo la Kabasha wamekimbia makazi yao.
Wakati huo huo jana Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa, una wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea hali ya vurugu na machafuko huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kusimamia amani baada ya kukamilisha safari yake ya siku tano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 
Jean-Pierre Lacroix amesema kuwa, vitendo vya kutumia mabavu na kuweko ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo ni mambo ambayo yanatia wasiwasi mkubwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.