Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewafikisha
mahakamani, mmiliki kampuni ya PAP, Habirnder Seth Singh na
mfanyabiashara James Rugemalira kwa makosa ya uhujumu uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa
Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola amesema, “Leo nawapa taarifa kuwa
tunawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, kwa makosa ya kuhujumu
uchumi na mengine yanayofanana na hayo.”
Amesema kwa muda mrefu amekuwa
akiulizwa kesi za Escrow na kampuni ya kufua umeme ya Independent Power
Tanzania Limited (IPTL) zimeishia wapi, hivyo taasisi hiyo imechunguza
shauri hilo kwa muda mrefu na kujiridhisha kwamba linaweza kufikishwa
mahakamani.
“Kwa hatua ya awali wataenda Mahakama ya Kisutu, baada ya hapo kuna
utaratibu wa kimahakama, watapelekwa mahakama maalumu kutokana na
kiwango cha hujuma kilichofanyika na fedha zilizohusika,” amesema
Mlowola.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.