ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 23, 2017

VIDEI:- KANISA LAENDA KUHIJI......Waamini wa dhehebu wa kanisa katoliki wametakiwa kuenzi na kuhifadhi maeneo ya kistoria ya kanisa hilo ili historia ya kanisa izidi kuwepo kwa vizazi vijavyo.

Katika safari ya hija ya kumbukumbu ya wamisionarai waliofika Afrika Mashariki wakianzia Tanzania na baadae nchini Uganda mahujaji hao wamesema ipo haja ya historia ya kanisa kuenziwa kwa kuboresha sehemu za historia.

Baada ya wamisionari kutoka Bagamoyo na Zanzibar walifikia hapa KAGEYE mkoani Mwanza  ili kueneza injili kwa kanda ya ziwa na baadae kuingia  nchi jirani Uganda, eneo hili la kageye linabaki kuwa chimbuko la kanisa hili.

Safari ya mahujaji hawa kutoka mkoa wa Mwanza kuelekea nchini Uganda ililenga kutembelea maeneo ya kihistoria ya kanisa katoliki wakianzia Kageye,Bukumbi mkoani Mwanza ambapo kanisa la kwanza la katoliki lilijengwa,  na baadae kuhitimisha na Namgongo nchi Uganda.Pause

Maeneo ya kihistoria ya kanisa inadaiwa kukosa muamko wa waamini kutembelea na kujifunza historia ya kanisa iliyoachwa na wamisionari walifika Afrika kueneza injili ya kikristo.Pause

Ni miaka 150 sasa ya ukristo tangu dini hii ingie Tanganyika baada ya wamisionari  roho mtakatifu kuingia Tanganyika tangu mwaka  1868 kupitia Bagamoyo na Zanzibar ili kueneza dini la kikristo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.