ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 28, 2017

TUME YA UCHAGUZI: WAANGALIZI 2,000 KUSIMAMIA UCHAGUZI UJAO WA RWANDA.

Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda imetangaza kuwa, waangalizi zaidi ya 2,000 watakuwa nchini humo kushuhudia uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika tarehe 4 mwezi Agosti.

Charles Munyaneza, Katibu Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi amewaambia waandishi wa habari kwamba, wanakadiria wasimamizi wa uchaguzi ujao watafikia 2000.
Amesema kuwa, miongoni mwa waangalizi hao ambao wamewasilisha maombi ya kupewa vibali ni mabalozi wa mataifa ya kigeni nchini humo na kwamba, wengine ni kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na waangalizi binafsi.
Hata hivyo, Umoja wa Ulaya tayari umeshatangaza kuwa, hautatuma waangalizi wake nchini Rwanda. Wakati uo huo, msemaji wa Mashirika ya kiraia nchini humo Jean-LĂ©onard Sekanyange, amesema watatuma waangalizi zaidi ya 200 kushuhudia Uchaguzi huo.
Kampeni rasmi za uchaguzi huo, zinatarajiwa kuanza tarehe 14 mwezi Julai na kumalizika Agosti tatu ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi wenyewe..
Rais Paul Kagame hatarajiwi kupata upinzani mkali katika uchaguzi ujao.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, jana Tume Huru ya Uchaguzi nchini Rwanda ilipasisha majina mawili tu ya wagombea wa kiti cha Rais kutokana na wagombea wengine wanne waliowasilisha fomu za kuwania nafasi hiyo kutotimiza masharti.
 
Waliopasishwa ni Rais Paul Kagame wa chama tawala cha RPF na Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa ya tume hiyo, wagombea wanne ambao hawakupasishwa jana wana muda hadi kufikia Julai 6 mwezi ujao wawe wamekamilisha masharti vinginevyo ni wagombea wawili tu watakaochuana katika kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi ujao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.