Mwenyekiti wa OJADACT,
akiongea na Waandishi wa Habari juu
ya msimamo wa chama kwa
kufungiwa Gazeti la Mawio , leo Jijini Mwanza
|
Neema Joseph
Mwanza.
Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita
Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania(OJADACT) walaani kufungiwa kwa
Gazeti la Mawio.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ofisi za
chama Mwenyekiti Bw, Edwin Soko amebainisha kuwa, OJADACT
wanalaani kufungiwa kwa gazeti
la Mawio, kwa kuwa makosa mawili yaliyoainishwa hayana
uzito wa kulifungia Mawio
kosa la kwanza Chini ya kifungu cha namba 59 chaa Sheria ya
Huduma za Habari 2016, kwa kuchapisha
picha za marais wastaafu na kuwahusisha na kashifa ya rushwa wakati tamko la
Rais lilikataza kujadiliwa kwa marais wataafu.
Kosa la pili Chini ya kifungu cha 38 cha
Sheria ya Huduma za Habari 2016, gazeti la Mawio linatuhumiwa kuwa lilichapisha
maagizo na maelekezo ya Serikali, lilinukuu kauli yambunge wa Singida Mashariki
Chadema Tundu Lissu.
Bwana Soko, alisema hawajaridhishwa na sababu zilizotolewa na Waziri wa Habari,
Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alioutoa Juni 15, 2017 na
kulifungia gazeti hilo.
“Hii
si mara ya kwanza kwa Gazeti la Mawio kufungiwa, Magazeti mengine yaliyowahi
kufungiwa ni, Mwananchi , Mawio, Mwanahalisi na mtanzania kwa kutumia Sheria ya
Magazeti ya mwaka 1976” Alisema Bwana Soko.
Akichambua makosa
hayo bwana Soko alisema
kuwa, Kwa mujibu wa kifungu cha 50
(a),(b),(c) ,(d) na (e) na 59 cha Sheria ya Huduma za Habari, mamlaka yenye
uwezo wa kufungia Gazeti ni Mahakama na sio Waziri baada ya kumsikiliza
mtuhumiwa , hivyo Waziri amekiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
anapaswa afunguliwa kesi ya kukiuka katiba ya
Nchi , pia wakati tamko linatoka gazeti la Mawio lilikuwa limekwisha
chapishwa hivyo halikupaswa kuchukuliwa hatua.
Pia aliongeza kuwa, Kwa mujibu wa kifungu cha 38 cha Sheria ya
Huduma za Habari halina mashiko kwa kuwa, Vyombo vya Habari vina nafasi ya
kunukuu mijadala na majadikiano yanayofanyika bungeni na kuyachapisha kwa lengo
la kufikisha kinachojadiliwa.
Huu ni unyimwaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari
na haki ya kupata taarifa, kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 18 ya Katiba ya
Nchi. Tunawaomba wadau na watanzania wote kuungana na kupinga maamuzi gandamizi
dhidi ya vyombo vya habari, Gazeti la Mawio lifungue kesi dhidi ya maamuzi ya
Serikali ya kulifungia. , Alisema Soko
Bwana
Soko ameiomba Serikali kufuata sheria za Nchi ili kuepuka migongano na Wadau wa Habari, pia iheshimu uhuru wa habari ni haki ya kikatiba kama ilivyoainishwa kwenye
ibara ya 18 ya katiba ya nchi yetu na kama ilivyoainishwa kwenye mikataba ya
kikanda, kimataifa, na kwenye mkataba wa
Azimio la Kimataifa la Haki ya binadamu 1948, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za
Kisiasa na Kiraia (ICCPR), chini ya ibara ya 19, Mkataba wa Aarhus, Azimio la
Uhuru wa kujieleza la Afrika 2002 na Azimio la Afrika Juu ya Demokrasia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.