ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 12, 2017

MUGABE AMTIMUA MWENDESHA MASHTAKA MKUU WA SERIKALI YAKE.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemtimua kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi hiyo kwa tuhuma za kuwa na mwenendo usiofaa. 

Gazeti la serikali ya harare la The Herald limetangaza kuwa, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali ya Zimbabwe, Johannes Tomana amefutwa kazi kutokana na mienendo isiyofaa na uzembe baada ya tume iliyoteuliwa na Mugabe kutaka afukuzwe. Gazeti hilo limeongeza kuwa, Johannes Tomana alikabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya ofisi na madaraka yake.

Johannes Tomana alisimamishwa kazi kwa muda mwezi Februari 2016 baada kutupilia mbali mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya watu wawili waliotuhumiwa kupanga njama ya kulipua bomu kwenye kiwanda cha maziwa linachomilikiwa na mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.

Rais Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe Duru za ndani ya Zimbabwe zinasema kuwa, sasa Johannes Tomana atakabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya madaraka yake.
 
Mivutano kati ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Zimbabwe na familia ya Rais wa nchi hiyo imekuwa ikiendelea kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.