ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 19, 2017

MTOTO ALIYEZALIWA NDANI YA NDEGE APEWA OFA YA KUSAFIRI BURE MAISHANI.

Shirika moja la ndege la kibinafsi nchini India limemtunuku safari za bure mtoto aliyezali ndani ya moja ya ndege zake, iliyokuwa safarini kutoka Saudi Arabia kuelekea nchini India.

Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama kujifungua mtoto umbali ya futi 35,000 angani.

Mama na mtoto wake walipelekwa hospitalini baada ya ndege ya Boeng 737 kutua katika mji wa magharibi wa Mumbai.

Kampuni iliwashukuru wahudumu kwa kumsadia mama kujifungua salama.

Shirika hilo lililisema kuwa ndiyo mara ya kwanza mtoto kuzaliwa kwenye ndege yake.

Lakini mashirika kadhaa yamekumbana na hali kama hiyo. Wahudumua wa shirika la ndege la uturuki walisherehekea kuzaliwa kwa mtoto msichana ndani ya ndege mwezi Aprili mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.