ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 8, 2017

MONGELLA AWAKOROMEA WANAOLALIA WAKULIMA WA PAMBA KWA KUNUNUA BEI PUNGUFU NA ILE YA SERIKALI.

Siku moja baada ya Bodi ya pamba tanzania kufungua msimu wa ununuzi wa zao hilo kwa wakulima wa mikoa 15 ya kanda ya Ziwa na Magharibi, serikali mkoani Mwanza imepinga bei ya shilingi 1100 iliyotangazwa na bodi hiyo na badala yake imeagiza kampuni zinazonunua zao hilo katika mkoa huo kuwalipa wakulima bei ya shilingi 1300 kwa kila kilo moja ya pamba.
 
Mjadala mkali umeibuka kati ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya pamba Tanzania Michael Mutunga kuhusu bei elekezi ya shilingi 1100 iliyokuwa imetangazwa na bodi hiyo,ambapo Mongella amesema serikali haiko tayari kujaribiwa na wanunuzi wa zao hilo. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA MHE.MONGELLA


Mwenyekiti wa kikao cha kujadili maendeleo ya sekta ya pamba mkoani Mwanza John Mongella, pia ameagiza wakuu wa wilaya kuwakamata na kuwafungulia mashitaka wanunuzi watakaoenda kununua pamba bila utaratibu wa kupitishwa na halmashauri husika.

Sakata la kampuni ya Alliance iliyoingia mkataba na wakulima wa wilaya ya Magu, ambayo inadaiwa kushindwa kuwasaidia wakulima kwa kuwakopesha mbegu na madawa ya kuulia wadudu wanaoshambulia zao la pamba, limetawala mjadala huo baada ya mkuu wa mkoa kuagiza kampuni hiyo isiruhusiwe kununua pamba wilayani humo kwa kushindwa kutimiza masharti ya mkataba huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.