ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 6, 2017

LOWASSA ATOA MANENO MAZITO MSIBANI.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA, Mh. Edward Lowassa amempongeza muasisi wa Chama hicho Mzee Mtei kwa kukutana na Mzee Ndesamburo na kutengeneza chama imara, huku akitoa ahadi ya chama hicho kuongoza mwaka 2020.

Akizungumzaa kwenye ibada ya kuuaga mwili wa Mzee Ndesamburo, Mh. Lowassa amesema kwamba  waasisi hao wameacha  chama chenye nguvu sana na ambacho kinafanya nzuri na kwa weledi.


"Nakupongeza Mzee Mtei kwa kukutana na Ndsamburo. Nakupongeza wewe zaidi kwa sababu umetuachia chama chenye nguvu. Pale nilikuwa namnong'oneza Mzee Mtei kwamba mwaka 2020 tutachukua ushindi,pamoja na jitihada zao mungu atatuongoza na tutaweza" - Mh. Edward Lowassa.


Akizungumzia kuhusu suala la polisi kuzuia eneo la uwanja wa Mashujaa kutumika kumuaga Mzee Ndesamburo, Mh Lowassa amefunguka kuwafariji wafiwa, wanachama na wananchi kwa kuwataka wasamehe yaliyotokea.


"Wamewakatalia uwanja wa Mashujaa lakini hapa kwenye uwanja wa majengo ndo pamejaa zaidi.Tuwasamehe bure au tuwaachie maneno ya biblia kwamba , Waacheni wafu wazike wafu wao maana hupimi watu kwa uwanja kujaa bali kwa mioyo yao na waliopo hapa ni wale waliompenda na kumuheshimu Mzee wetu" - Mh. Lowassa alifunguka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.