ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 13, 2017

KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA HAI IMEVAMIA SHAMBA LA MBOWE??

Screenshot from 2017-06-13 17-08-40.png
INADAIWA KUWA: Kamati ya usalama ya Wilaya ya Hai ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, imevamia Shamba La Mbogamboga linaloendeshwa na Freeman Mbowe na kufanya uharibifu.

Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Hai ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa wamevamia shamba la mbunge wa jimbo hilo, Mh. Freeman Mbowe lililoko nyumbani kwake Machame na kuharibu miundo mbinu na mali pamoja na mboga mboga na mimea.

Mh. Mbowe amezungumza moja kwa moja kutoka bungeni mjini Dodoma... "Ni kweli nimezipata hizi habari mkuu wetu wa wilaya akiambatana na askari na waandishi wa habari walikwenda kwenye mradi wetu na kukatakata mimea na kufanya uharibifu mkubwa, taarifa nilizozipata kutoka kwa wafanyakazi waliopo site walisema walipokea barua kutoka NEMC kuwa kilimo tunachokifanya kinaharibu mazingira na hatukustahili kuendelea na kilimo kile, ni jambo la kufedhesha sana tunawahamasisha watanzania wawekeze kwenye kilimo cha kisasa lakini viongozi wa serikali bila kuheshimiana wanakwenda kuharibu, sio kweli kilimo chetu hakiharibu mazingira, familia yetu imelima kwenye shamba hilo kwa zaidi ya miaka 80"


Screenshot from 2017-06-13 17-06-29.png

Screenshot from 2017-06-13 17-06-19.png

Screenshot from 2017-06-13 17-05-53.png
PICHA KWA HISANI YA JAMII FORUM.​
LAKINI BADO BLOGU HII (GSENGO BLOG) YA JAMII INAENDELEA KUCHUNGUZA TAARIFA HIZI KUPATA UNDANI NA PUNDE TUTAPATA UTHIBITISHO TOKA KAMATI INAYO RUSHIWA TUHUMA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.