ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 1, 2017

KAMANDA MWANDAMIZI WA AL-SHABAAB AJISALIMISHA KWA SERIKALI SOMALIA.

Kamanda mmoja mwandamizi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab amejisalimisha kwa jeshi la taifa la Somalia.

Kamanda mkuu wa jeshi la Somalia, Jenerali Ahmed Mohamed Tredishe amesema mwanachama huyo wa al-Shabaab anayejulikana kwa jina Bishar Mumin Afrah amejisalimisha kwa jeshi hilo katika mji Buloburte eneo la Hiran, yapata kilomita 200 kaskazini mwa Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Inaarifiwa kuwa, kamanda huyo mwandamizi wa genge la kigaidi la al-Shabaab amejisalimisha kwa vyombo vya usalama sambamba na kukabidhi bunduki mbili aina ya AK47 na shehena ya risasi.
Hivi karibuni Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo alitoa msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo wa al-Shabaab ambao wataweka silaha chini na kujisalimisha kwa serikali.
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia.

Mapema mwezi uliopita wa Mei, Wizara ya Habari ya Somalia ilisema kuwa, Moalim Osman Abdi Badil, kamanda wa ngazi za juu wa al-Shabaab pamoja na wanamgambo wengine watatu wa genge hilo waliuawa katika mapigano na jeshi la Somalia kwenye eneo la Shabelle ya Chini.
Katika hatua nyingine, walimu wawili wa Kenya wameripotiwa kutekwa nyara na wanamgambo wa al-Shabaab katika mji wa Fafi kaunti ya Garissa usiku wa kumkia leo baada ya magaidi hao kuteketeza moto shule moja katika eneo hilo la kaskazini mashariki. Kadhalika magaidi hao wameng'oa na kuiba mlingoti wa mawasiliano ya simu ya mkononi (rununu) katika eneo hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.