ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 27, 2017

IRAN YATAKA MASHINDANO YA SILAHA MASHARIKI YA KATI YASITISHWE.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema kuna haja ya kuwepo jukwaa la kustawisha mazungumzo baina ya nchi za Ghuba ya Uajemi huku akitoa wito kwa nchi za eneo hili kusitisha mashindano yao ya silaha.
Akizungumza mjini Berlin Ujerumani Jumatatu katika Baraza la Sera za Kigeni la Ulaya, Zarif amesema mashindano ya silaha Mashariki ya Kati yanatokana na uhusiano wa nchi za Magharibi na baadhi ya nchi za eneo.

Aidha Zarif ametoa wito kwa nchi za Ulaya kutumia ushawishi wao kupungua mzozo katika Ghuba ya Uajemi ambao umeibuka baada ya Saudi Arabia kuchochea waitifaki wake kukata uhusiano na nchi jirani ya Qatar.

Emir wa Qatar Sheikh Tamim Aal Thani
Saudi Arabia, Bahrain, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu zimekata uhusiano wa kidiplomasia na Qatar na pia kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa nchi kavu, angani na baharini. 
 
Nchi hizo zimedai kuwa Qatar inaunga mkono ugaidi na kuvuruga uthabiti katika eneo madai ambayo wakuu wa Doha wameyakanusha.  
 
Zarif amesema nchi hizo ambazo zinaituhumu Qatar kuunga mkono ugaidi pia zimetoa tuhuma hizo zisizo na msingi dhidi ya Iran lengo likiwa ni kufunika kufeli kwao katika kukidhi mahitaji ya watu wao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.