ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 20, 2017

HII NDIYO AJALI ILIYO ONDOSHA UHAI WA SHABIKI DAMU WA YANGA MAARUFU 'ALLY YANGA'

Ajali hii imetokea barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro mtu mmoja amepoteza maisha hapo hapo. Aliyefariki ni mshabiki  maarufu wa timu ya Yanga, anaitwa Ally Yanga


MWANACHANA wa klabu ya Yanga na mpenzi maarufu wa soka nchini, Ally Mohamed anayejulikana zaidi kwa jina la utani ‘Ally Yanga’ amefariki dunia leo baada ya ajali ya gari iliyotokea, eneo la Mpwapwa, Dodoma. 

Taarifa zinasema Ally Yanga alikuwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge kabla ya kupata ajali hiyo barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro na kufariki hapo hapo. Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam. 

WAKATI HUO HUO:-
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha shabiki huyo maarufu wa Yanga, Ally Mohamed aka Ally Yanga kilichotokea leo katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampun ya Fanikiwa ambalo lilikuwa kwenye promotion na sio kwamba alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.

Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.