ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 28, 2017

HATIMAYE NGOMA ASAINI YANGA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC.

Ngoma aliwasili jana usiku Dar es Salaam baada ya taarifa kwamba alikuwa anahitajika na klabu ya wekundu wa msimbazi simba na huku kukiwa na tetesi kwamba anaendelea kukipiga katika kikosi cha Yanga.

Lakini tangu jana mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga kabla ya leo mchana kusaini, hivyo pia kuzima tetesi za kwamba anataka kujiunga na mahasimu, Simba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.