ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 3, 2017

PART ONE:- BONANZA LA KIPINDI CHA MICHEZO JEMBE FM 'SPORTS RIPOTI' LILIVYOAMSHA JIJI LA MWANZA.

Kikosi cha Jembe Fm kabla ya kushuka dimbani kupepetana na Gold Krest Fc na kutolewa katika mchezo wa mtoano baada ya kunyukwa bao 3-1 Katika dimba la Nyamagana jijini Mwanza, Bonanza la kutimiza miaka miwili ya kipindi cha 'SPORTS RIPOTI' ya Radio Jembe Fm.
Kikosi cha Gold Krest Fc Katika dimba la Nyamagana jijini Mwanza, Bonanza la kutimiza miaka miwili ya kipindi cha 'SPORTS RIPOTI' ya Radio Jembe Fm.
Kikosi cha Mkolani Fc.
Kikosi cha Bodaboda Fc.
Mtafutano.
Mashambulizi.....dah....dah....dah
Mtangazaji wa Sport Ripoti ya Jembe Fm Vanessa akitimbwirika na ratiba ndaniya Bonanza.
Mkolani baada ya kuwaondosha Bodaboda.
Moja kati ya mitanange iliyokuwa na ushindani wa kweli ni kati ya Mkolani dhini ya Bodaboda kuwania ubingwa wa Sports Ripoti Bonanza Cup 2017.
Kasi,ufundi na umakini vilitawala.
Mtu na mtu......
Moja kati ya vinogezho ilikuwa ni burudani kutoka kwa meza ya Jembe DJz wakuitwa Deejay Kflip hapa akifanya yake.
Mmoja wa wachezaji toka Mkolani Veteran akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Mwana All Star Veteran.
Hapiti mtu....
Aksante Mwanza kuitikia katika Bonanza la Sports Ripoti ya Jembe Fm.
Ukisikia kuuzwa ndiyo huku.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege (kushoto) akifuatilia mchezo pamoja na Mgeni Rasmi
Tigo walishiriki vyema katika Sports Ripoti kuadhimisha miaka miwili, sherehe zilizofanyika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na kufana.
Wakali wa 'Town' Mjengoni Fc katika picha kabla ya mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Tigo.
Tigo Fc walipata bao kunako dakika za awali tu za mchezo, hata hivyo Mjengoni Fc walifanikiwa kurudisha goli hilo na mchezo kwenda kwenye hatua za matuta.
Mtu na mtu........

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.