ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 19, 2017

AMNESTY INTERNATIONAL YAITAKA MISRI IACHE KUTEKELEZA HUKUMU YA KIFO.

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limevitaka vyombo vya mahakama nchini Misri viache kutekeleza hukumu ya kunyongwa raia saba wa nchi hiyo wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limetoa taarifa likitaka kutazamwa upya kwa hukumu ya raia saba wa nchi hiyo waliohukumiwa kunyongwa. Shirika hilo limetaka kurejeshwa mafaili ya watuhumiwa hao katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo ili ipitie upya hukumu hiyo.
Sehemu moja ya taarifa ya Shirika la Msamaha Duniani imebainisha kwamba, kufanyiwa marekebisho sheria inayozuia kukatiwa rufaa hukumu ya kifo ambayo hivi karibuni iliidhinshwa na rais Abdul Fatah al-Sisi ni jambo ambalo linaweza kupelekea kuongezeka hukumu kama hizo na kunyongwa raia wa nchi hiyo.
 Mahakama ya Misri
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Jumamosi Mahakama moja nchini Misri iliwahukumu adhabu ya kifo watu 31 kwa tuhuma za kushiriki katika mauaji ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
 
Kwa miaka kadhaa sasa Misri imekuwa ikikabiliwa na machafuko, mauaji, maandamano na mashambulizi katika pembe mbali mbali za nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, hasa baada ya tarehe 3 Julai, 2013 wakati jeshi la nchi hiyo lilipofanya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Mohammad Morsi, rais wa kwanza wa Misri kuchaguliwa kidemokrasia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.