ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 7, 2017

ALIYE VUNJA OFISI ZA IDARA YA MAJI WILAYA YA UKEREWE NA KUPORA MIUNDOMBINU NA NYENZO ANASWA NA JESHI LA POLISI MWANZA.



TAREHE 07/06/2017 MAJIRA YA SAA 04:15HRS Alfajiri katika mtaa wa Bukongo wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza, askari wakiwa kwenye doria walifanikiwa kumkamata Daris Athumani @ MTAA WA SABA, mwenye umri wa miaka 27, mkazi wa kijiji cha Bulima akiwa na koki 68 za maji, stoper 04, joint za koki 07 za maji, key board ya computer 01, monitor 01, cpu 01, na printer 01, mali za ofisi ya idara ya maji ya Halmashauri ya wilaya ya Ukereweambazo alivunja na kuiba usiku ofisini hapo, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
 
Awali askari wakiwa kwenye doria katika maeneo ya mji wa nansio walipokea taarifa kutoka kwa wasiri kwamba katika ofisi ya Idara ya maji wilayani hapo wapo watu ambao wanafanya uhalifu, basi kutokana na taarifa hizo baadhi ya askari waliweka mtego katika barabara zinazoelekea maeneo hayo kisha wengie wakafanya ufuatiliaji wa haraka hadi ofisini hapo, ndipo baadaye mtuhumiwa Dalis Athumani alikamatwa maeneo ya Bukongo akiwa na vitu tajwa hapo juu mali za Ofisi ya Idara ya Maji.

Polisi wapo katka upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. 

Aidha polisi wanaendelea na msako pamoja na upelelezi wa kuwatafuta watu wengine walioshirikiana na mtuhumiwa katika uhalifu huo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa kwa ujumla hususani wamiliki wa taasisi za serikali na watu binafsi akiwataka kuwa na utaratibu wa kuweka walinzi katika ofisi zaoili kuweza kudhibiti wahalifu wa aina kama hii mapema kabla hawajaleta madharakatika ofisi zoa.

Pia anawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa mapema na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.