ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 17, 2017

YANGA Sc WASAINI DILI LA BILIONI 5 LEO MEI 17, 2017

Leo Mei 17, 2017 KLABU ya Yanga imevuna dau la Bilioni 5  zaidi ya mahasimu wao, Simba SC  waliosaini dau la Sh. Bilioni 4.96 katika udhamini wa kampuni ya SportPesa. kwa miaka hiyo hiyo mitano.

Akizungumza wakati hafla ya kusaini mkataba huo makao makuu ya Yanga, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani mjini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kwamba wameingia mkataba huko kwa dhumuni la kuendeleza soka katika kufikia malengo ya klabu hiyo.

 Tarimba ameongeza kuwa fedha hizo zitatolewa kwa awamu, mwaka wa kwanza, Yanga watapata Sh. Milioni 950 na kama ilivyo kwa Simba, klabu ya Jangwani pia itatakiwa kuthibitisha matumizi ya fedha hizo kama yamefanyika kwa shughuli za maendeleo ya soka.

Alisema licha ya mkataba huo, pia kutakuwa na motisha ambapo wakishinda ubingwa wa Ligi Kuu watapewa zawadi ya Mill. 100.

“Pia ikishinda michuano kama Kagame pia watapewa zawadi na wakifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika watapata zawadi ya Mill. 250,”alisema Tarimba.
Ukiondoa kuzidiwa kidogo kwa dau, lakini kwa ujumla mkataba huo hautofautiani sana na wa Simba.

Lakini kikubwa ni kwamba kwa mara nyingine, vigogo wa soka Tanzania na mahasimu wa jadi, Simba na Yanga wanatarajiwa kuwa chini ya udhamini mmoja tena, baada ya awali wote kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kati ya mwaka 2007 na 2016.

TBL iliachana na Simba na Yanga na kwa ujumla ilijitoa kwenye kudhamini soka, hadi timu ya taifa, Taifa Stars kufuatia mabadiliko ya umiliki wa kampuni hiyo.
Na miezi michache baada ya kupoteza udhamini wa TBL kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, hatimaye Simba na Yanga zitakuwa zinavaa jezi zenye kufanana tena maandishi kifuani, SportPesa.

CHANZO: BIN ZUBEIR.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.