ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 17, 2017

WAKUU WA MIKOA TISA WA KANDA YA MAGARIBI WANAOLIMA PAMBA WATEMBELEA SHAMBA LA MBEGU BORA.

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba TANZANIA Marco Mtungo.
 NA ZEPHANIA MANDIA

Wakuu wa mikoa tisa ya kanda ya ziwa wanaolima Pamba wametembelea mashamba ya mfano yanayolima mbegu bora ya Pamba katika kijiji cha mwabusalu wilaya meatu  Mkoani Simiyu.

Mkoa mkuu wa mkoa wa mwanza John mongela,ameyasema hayo wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa walipotembelea mashamba ya uzalishaji mbegu bora,Mkoa wa mwanza unatarajia kupata kiasi cha Tani 25000 kwa mwaka 2017 kutoka Tani 7000 za mwaka jana huku ukiwa ni mkakati wa mwanzo wa makubaliano baina ya mikoa inayolima pamba nakuhakikisha wanafufua zao la pamba ili kukidhi mahitaji ya soko la pamba ambalo ndio zao kubwa la biashara ndani na nje ya nchi.

Ata hivyo wakuu wa mikoa hiyo  Geita,Kagera,Kigoma,Singida,Tabora,Shinyanga,Simiyu,na Mwanza wameamua kufikia  makubaliano baina ya wakulima pamoja na viongozi wa bodi ya pambaili kuhakikisha wanaingia katika mikataba mizuri ya kilimo cha mkataba  huku kauli mbiu ikiwa Pamba ni dhahabu Nyeupe.

 

Pamoja na juhudi zinazofanywa na serekali,Mkurugenzi wa bodi ya pamba Tanzania Marco mtunga,amesema kuwa kutokana na mbegu bora ya pamba inayolimwa mwabasalu meatu kufikia mwaka 2019 na 2020,tatizo la mbegu litakua limekwisha.

 Nao baadhi ya wakuu wa mikoa waliotembelea  mashamba ya wakulima pamoja na shamba la mfano la kamati ya ulinzi na usalama  na wakuu wa idara ya wilaya ya kwimba ambalo limefanya vizuri katika majaribio ya kilimo cha pamba wakatoa maoni yao.

Wakulima wa Pamba wilayani Kwimba wameiomba serikali kuhakikisha wasambazaji wa pembejeo wa zao hilo kuleta madawa yenye uwezo wa kuuwa wadudu tofauti na hali ilivyo wakati huu ambapo wametumia dawa zaidi na kuyasababishia hasara mashamba yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.