ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 22, 2017

UNFPA NA WIZARA YA AFYA ZAJIPANGA KUTOKOMEZA FISTULA NCHINI ALBOGAST B. MYALUKOFISTULA ni moja ya magonjwa yanayohatarisha afya ya mama mjamzito na mtoto kutokana na madhara yake endapo huduma ya haraka haitapatikana wakati wa kujifungua. United Nations Populations Fund UNFPA nchini Tanzania pamoja na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  kwa pamoja vimeungana kuhakikisha ugonjwa huo unabaki historia nchini.

Kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kutokomeza Fistula ambayo huadhimishwa Mei 23 kila mwaka, Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto, Ummy Ally Mwalimu ameitaka jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi za afya zinazotoa huduma ya matibabu ya Fistula. 

Waziri Ummy  ameihakikishia jamii kuwa serikali kupitia vizara yake imejipanga kuboresha vituo vya afya 100 nchini ili viweze kutoa huduma ya upasuaji ya dharura kwa wajawazito. Pia ameiasa jamii kuepuka vitendo vya ubaguzi kwa wagonjwa wa Fistula.

UNFPA kupitia kwa mwakilishi wake nchini Hashina Begum, imesema itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wake kama Amref Health Africa kuhakikisha huduma ya matibabu ya Fistula inawafikia wote wenye matatizo. Hadi sasa UNFPA imefanikisha matibabu kwa jumla ya  wanawake 85 elfu duniani kote.


Aidha Mkurugenzi Mkuu wa CCBRT Erwin Talemans, amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa kuwafikisha wagonjwa katika vituo vinavyotoa huduma ya tiba hiyo ikiwemo CCBRT Dar es Salaam na Bugando Mwanza pamoja na Hospitali zingine nchini kama Mkinga iliyopo Tabora. Matbabu ya Fistula yanatolewa bure pamoja na gharama zingine kama usafiri na Chakula.


FISTULA INATIBIKA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.