ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 2, 2017

TRUMP: NIPO TAYARI KUKUTANA NA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI.


Huku mgogoro ukiendelea kushtadi kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa, yupo tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un
Trump ameyasema hayo katika mahojiano na jarida la Bloomberg na kusema kuwa, ikiwa atakutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un hiyo itakuwa fakhari kubwa kwake. Amesisitiza kuwa, ikiwa kutaandaliwa mazingira kwa ajili ya mkutano huo, yeye yupo tayari kabisa kukutana na kiongozi huyo kijana wa Korea Kaskazini.

Trump na Kim Jong-un
Rais Donald Trump ameongeza  kuwa na hapa ninamnukuu: “Wanasiasa wengi hawawezi kuzungumza matamshi kama haya, lakini mimi ninasema wazi kwamba, nitakutana na Kim Jong-un ikiwa kutaandaliwa mazingira.” Mwisho wa kunukuu. Rais Donald Trump wa Marekani ametamka hayo katika hali ambayo, harakati za kijeshi za Washington katika Peninsula ya Korea, zimeshadidisha mgogoro katika eneo hilo kiasi cha kuifanya serikali ya Korea Kaskazini kuongeza harakati zake za silaha za nyuklia na makombora ya balestiki kwa ajili ya kukabiliana na vitisho hivyo vya Marekani. 

Hii ni katika hali ambayo, kwa mara nyingine serikali ya Korea Kaskazini imeitahadharisha Marekani kwamba, ikiwa meli za kivita za nchi hiyo zitaendelea kukaribia maji yake katika Peninsula ya Korea, basi itaziangamiza silaha za nyuklia za Washington na kuzigeuza kuwa vyuma chakavu.

Katika hatua nyingine, Pyongyang imetangaza kuwa, katika kufuatilia siasa za uhasama za Marekani na washirika wake, hususan Korea Kusini na Japana, imekusudia kujizatiti kwa silaha za nyuklia ili isiweze kushambuliwa kama ilivyoshambuliwa nchi ya Syria. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini, Pyongyang imeazimia kuunda kwa haraka sana silaha nyingi za nyuklia ili kukabiliana na vitisho vya Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.