ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 10, 2017

SALUM MWALIMU AMTUMIA RAIS JPM, MAJALIWA NA MBOWE KUJINADI UCHAGUZI EALA.

Mgombea wa uwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kwa upande wa Chadema, Salum Mwalimu ametumia jina la Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kujinadi.

Wakati akihitimisha maombi yake ya kura baada ya kuulizwa maswali matatu na wabunge, Mwalimu amesema atakapovuka mpaka wa Tanzania kuiwakilisha katika mataifa mengine kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki endapo atachaguliwa atakuwa mwakilishi wa Taifa na si chama.

Mwalimu amesema hata akivuka mpaka Rais ni (John) Magufuli, Waziri Mkuu ni(Kassim) Majaliwa na (Freeman) Mbowe atabaki kuwa mwenyekiti wa chama, hivyo kuwahimiza wabunge kumchagua bila kujali itikadi za chama.

Wagombea wengine wa nafasi hiyo kwa Chadema ni Profesa Abdallah Safari, Pamela Massay,  Ezekia Wenje, Lawrence Masha  na  Josephine Lemoyan

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.