ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 16, 2017

YANGA UBINGWA VPL UKO SEBULENI.

Ushindi wa Yanga wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africans unaifanya Yanga kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kufikisha pointi 68 sawa na Simba lakini Yanga wanarejea kwenye nafasi ya kwanza kutokana na wastani wa magoli.

Ikiwa imebaki mechi moja kabla ya ligi kumalizika, Simba inahitaji kushinda mechi yao dhidi ya Mwadui FC kwa magoli mengi halafu Mbao nayo iifunge Yanga kwa idadi kubwa ya magoli ili Simba itwae taji la VPL kitu ambacho ni kigumu kulingana na hali ilivyo kwa sasa.

Haikua rahisi kwa Yanga kupata ushindi dhidi ya Toto kwa sababu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilikua hazijafungana.


 Goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa na Amis Tambwe dakika ya 81 ya mchezo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.