ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 15, 2017

MTI WA MAAJABU WAGOMA KUKATWA JIJINI MWANZA....!!
"Leo Nimeshuhuhudia wananchi wa Pansiansi jijini Mwanza wakiwa wamefurika kuushuhudia mti unaodaiwa kuwa wa maajabu, eti ulikua unaondolewa kupisha ujenzi wa barabara iendayo airport."

Wanadai ETI ulipokua unakaribia kuondoleea na Grader Mti huo ukaongea na kusema.."Mniache hapa siendi kokote.." Mashuhuda wote waliofika hapo na kuwauliza, hakuna aliyethibitisha kuona kwa macho na kuthibitisha kwa sikio lake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Kila mtu alisikia tu taarifa hizo.... Wamejaribu eti kuukata na shoka utaongea.. wapiiii.. Kwa mujibu wa mashuhuda waliozuka mahala hapo wanadai mti huo una sauti ya kiume hivyo ni Babu na upo mwingine una sauti ya kike ambao ni Bibi.. 

Na kwamba eti Mti ulipokatwa ulitoa cheche na baadae ukatoa damu... dah .. "Nikacheka tu na kusema, kazi tunayo" Je wewe unaamini Nguvu za Giza?? 

Funguka muujiza unaoujua kama kweli..Simulizi by ndugu mwandishi @jembenijembe

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.