ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 17, 2017

MIZIZI, MATAWI, UDONGO, MAGOME YA MTI WA AJABU MWANZA SASA YAGEUKA KUWA DILI.

Ni siku ya pili mara baada ya mti wa maajabu jijini Mwanza uliopachikwa jina la *MTI WA JEMBE* kung'olewa, na sasa mizizi yake, matawi yake hata magome ya mti huu yamegeuka kuwa dili kwa wananchi, kama pichani inavyoonekana mmoja wa akina mama akibanjua magome ya mti huo kwaajili ya dawa......Mambo ya imani haya.
Baadhi ya watu wameonekana kufika eneo la mti huu na kufukia sarafu za fedha kwenye kifusi cha udongo uliofukuliwa toka kwenye mti huo na hatimaye kurundikwa pembezoni mwa barabara huku wengine wakichota udongo huo wakidai kuwa una bahati.
Kwa karibu moja ya sarafu zilizo tupwa kwenye udongo husika.
Mashuhuda wakizungumza juu ya kinachoendelea. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Kwa ukaribu zaidi mizizi ikihifadhiwa ndani ya mfuko wa safleti na mwananchi.
Emmanuel Mogenge huyu ni Afisa usalama mahala pa kazi kupitia kampuni yenye kandarasi kwa ujenzi wa barabara ya Makongoro - Airport. Hapa anazungumzia jinsi hali ilivyokuwa siku ya tukio na mauzauza anayokutana nayo kila kukicha.  
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Matawi dili, mizizi dili, udongo dili mwananchi n fuko lake.
Kifusi cha udongo wa mti husika.
Yako wapi Magome ya mti huu.....?
Ujenzi wa barabara unaendelea.
Barabara
Udongo unaondoshwa eneo ulipokuwepo mti.
Barabara na kando kando ya barabara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.