ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 23, 2017

MILIONI 250 ZA SPORTPESA KUIPA SINGIDA UNITED UBINGWA WA VPL


Na Abog
Baada ya kampuni ya michezo ya kubahatisha kutoka nchini Kenya SportPesa kumwaga zaidi ya bilioni 10 kwa vilabu vya Simba na Yanga, leo Mei 23 kampuni hiyo imetua rasmi katika klabu ya Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari kwenye Hotel ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Uwezeshaji wa kampuni hiyo Abbas Tarimba, amesema kuwa wana matumaini klabu hiyo italeata changamoto kubwa kwenye ligi msimu ujao. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Mkataba huo una thamani ya shilingi milioni 250, kwa msimu mmoja wa ligi ambapo wanatarajia kuongeza endapo timu hiyo itapata matokeo mazuri kwenye ligi msimu wa 2017/18. Pia kuna makubaliano maalum ya nyongeza (Bonus) endapo klabu hiyo itafuzu michuano ya kimataifa msimu ujao.

Kwa upande wa Singida United wamesema wana mipango ya kufanya vizuri kwenye ligi ndio mana wameanza na usajili mzuri wa kocha pamoja na wachezaji kutoka vilabu vikubwa barani Afrika kama Mamelodi Sondowns. 

Moja ya watu waliopo kwenye benchi la ufundi la Singida United ni nahodha Nizar Khalfan ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga pamoja na kocha Hans Van Pluijm ambaye naye amewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.