ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 23, 2017

MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UWT WILAYANI SENGEREMA YAFANYIKA.Mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa uwt wilaya ya Sengerema ambae pia ni diwani mstaafu viti maalumu kwa tiketi ya CCM yamefanyika JANA katilka kijiji cha Nyabutanga katika Halmashauri ya Buchosa .


Akizungumzia wasifu wa marehemu Stefania Shindika  katibu wa CCM mkoa wa Mwanza mwl Raymond Steven Mwangwala  amesema kuwa chama  kimempoteza mtu muhimu kwakuwa alikuwa mstari wa mbele kuwaunganisha wanawake katika wilaya ya Sengerema 
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Kwa upande wake m/kiti UWT mkoa wa Mwanza bi ELEN MAKUNGU amesema kuwa marehemu Stefania Shindika alikuwa chachu ya maendeleo kwa wanawake wa mkoa wa Mwanza.


Marehemu  Stefania Shindika  alizaliwa mwaka  10/10/1958 katika kijiji cha Kimuli wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, na amewahi kufanaya kazi katika CHAMA CHA USHIRIKA WA WAKULIMA (NYANZA) , mwaka 1975 alijiunga na chama cha Tanu na kasha kuhamia CCM mwaka 1977 ,mwaka 2005 marehemu Stefania alichaguliwa kuwa diwani viti maalumu kata ya nyakalilo mwaka 2012 alichaguliwa kuwa m/kiti UWT  wilaya ya Sengerema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.