ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 9, 2017

KWA SASA MAFUTA YANASAKWA KAMA DHAHABU NCHINI BURUNDI.

Na nchini Burundi uhaba wa fuel kwa ajili ya vyombo vya usafiri umeendelea kushuhudiwa licha ya serikali ya Bujumbura kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kupitisha sharia mpya za ugavi wa nishati hiyo.


Kutokana na hali hiyo, bei za usafiri nayo imeonekana kupanda kinyume na ilivyozoeleka. Hayo yanajiri katika hali ambayo, machafuko ya kisiasa yanatajwa kupungua kwa kiasi, ikilinganishwa na kipindi cha miaka miwili iliyopita, hasa baada ya kuibuka mgogogro wa kisiasa uliosababishwa na hatua ya Rais Nkurunziza kugombea kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais uliopita.
Foleni zikiendelea kushuhudiwa katika vituo vya uuzaji mafuta Burundi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.