ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 22, 2017

MKASA WA KUTUPWA MTOTO BARABARANI WILAYANI SENGEREMA


Wakati taifa bado linakumbuka matukio mbali mbali likiwemo la ajali ya wanafunzi na kuzama kwa meli ya mv Bukoba, wazazi wawili wilayani Sengerema waliofahamika kwa  majina  Kayungilo baba wa mototo na mama Azizi  mama wa mtoto wamejikuta mikononi mwa polisi baada ya tukio la mama huyo kumwacha mtoto Azizi kando ya barabara na kuondoka.

Akiongea na Jembe fm mama wa motto huyo amesema chanzo ni kutokupewa mahitaji ya motto kutoka kwa baba wa motto huyo ambae ni bwana Koyungilo.
MSIKILIZE Mama AZIZI.
Kwa upande wao mashuhuda wa tukio hilo wanesema kuwa baada ya kuwaona wazazi hao wakizozana kwa buda barabarani hapo ndipo waliwaona wakimweka mtoto Azizi kando ya barabara kumwacha na kumwakisha kuondoka na ndipo walipomkamata na kutoa taarifa polisi kwa msaada zaidi.
SIKILIZA Mashuhuda
HABARI NA OSCAR KAHUKA  JEMBE FM SENGEREMA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.