ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 31, 2017

KATIBU WA CCM MKOA WA ARUSHA ANUIA KUISAFISHIA NJIA CCM ARUMERU.

Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ernest Mpanda akizungumza katika kikao cha kuimarisha Utendaji  katika Halmashari ya wilaya ya Arumeru.Mbele ya watendaji mbalimbali wa Ofisi za Halmashauri hiyo mapema leo.
Mkuu wa wiaya ya Arumeru Alexander Mnyeti akizungumza katika kikao cha kuimarisha Utendaji  katika Halmashari ya wilaya ya Arumeru. Mbele ya watendaji mbalimbali wa Ofisi za Halmashauri hiyo mapema leo.
Mkuu wa wiaya ya Arumeru Alexander Mnyeti hapa alikuwa akisisitiza jambo juu ya utendaji akiwataka watendaji waHalmashauri ya wilaya yake kuitendea haki dhamana waliyopewa kama ajira toka serikalini, akisitiza pia wajibu wa kuzingatia muda wa kazi, uaminifu na kutatua changamoto za wananchi.
Sehemu ya watendaji waliojitokeza hii leo toka idara na vitengo mbalimbali wa Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Arumeru wakiwemo wenyeviti wa mtaa mapema leo.
"Tumefanya tathimini na kugundua kuwa sisi CCM kuna mahali tulikosea. Na kukiri mapungufu si kujidhoofisha bali ni kujiimarisha. Ni kama mgonjwa anayewahi kwa daktari baada ya kuziona dalili za ugonjwa, akipata tiba, huyo si mgonjwa tena. Mtu makini anajitathimini, anajiangalia na kisha anasonga mbele" 

Ni kauli ya Ernest Mpanda Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wa Ofisi za Halmashauri y Arumeru wakiwemo wenyeviti wa mitaa.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.