ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 2, 2017

GENGE LA DAESH LAUA RAIA 10 IRAQ KWA KOSA LA KUKATAA KUSHIRIKIANA NALO.


Wanachama wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh, wamewaua raia 10 katika mkoa wa Nainawa (Nineveh) nchini Iraq.
Shirika la Habari la Sumaria News limeripoti kuwa, magaidi hao wameenedelea kutenda jinai dhidi ya binaadamu nchini humo kwa kuwanyonga raia 10 ambao walikataa kushirikiana nao. Kabla ya hapo pia wanachama wa kundi hilo waliwaua raia wengine 50 huko magharibi mwa mji wa Mosul kwa kosa hilo hilo.

Magaidi hao wakiwapeleka vijana waliolipinga genge hilo kwenda kuuawa.
Tangu genge hilo liudhibiti mji wa Mosul mwaka 2014, limewanyonga karibu raia 1000 wa mji huo. Habari nyingine ni kwamba, kundi hilo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu, limeharibu maktaba ya chuo kikuu cha mji wa Mosul iliyokuwa na hadhi ya kimataifa na maarufu sana ambayo ilikuwa na zaidi ya vitabu laki moja na iliyosajiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).
Miongoni mwa jinai za magaidi wa Daesh
Awali maktaba hiyo ilishambuliwa na ndege za kivita za Marekani kwa kisingizio cha kupambana na wanachama wa kundi hilo ambao walikuwa wamekidhibiti chuo hicho, hujuma ambayo ilisababisha uharibifu mkubwa. Chuo kikuu hicho kilikuwa kinahesabika kuwa kitivo cha pili cha kielimu nchini Iraq.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.