ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 7, 2017

FULL TIME: ARSENAL YAIDUNGUA 2-0 MAN UNITED

 NA GSENGO JEMBE FM
Goli kutoka kwa Granit Xhaka na Danny Welbeck yalitosha kuifanya Arsenal kuweka rekodi yao mpya kushinda dhidi ya Jose Mourinho ambaye kamwe siku za awali hawakuweza kummudu. 

Kingine kizuri ni kwamba mchezo huu unaibua matumaini ya kumaliza ligi wakiwa nafasi nne za juu kitu ambacho ni kiu kwa timu zote kubwa.

Pamoja na ushindi huu Arsenal wanasalia katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, lakini sasa wanasalia pointi 6 nyuma ya Liverpool, pointi sita tena nyuma ya Manchester City na mbili tu nyuma ya Manchester United. 

Lakini mzigo haujamalizika huu babake kwani presha inazidi kuwa kubwa, na sasa wanakibarua cha kuwabanjua Southampton siku ya jumatano, ile hali United, wao wakivunjiwa mwiko wa  kushuka dimbani bila kufungwa tangu mwezi October hadi hii leo, Man United wanaweka kando hisia za kufuzu Ligi ya Mabingwa na inaonekana matumaini yao yamefifia huko wakielekeza nguvu zao kwenye kufuzu Ligi ya Uropa. 

Ni ukweli usiopingika kuwa Mourinho, kaupania mchezo wa marudiano wa Alhamisi dhidi ya Celta Vigo. They’ll take losing this one as long as they’re in Stockholm on 24 May. Thanks for reading and emailing.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.